Asasi na mashirika yalalamikiwa kukuza takwimu za maambukizi ya UKIMWI

Asasi zisizo za kiserikali na mashirika ya ndani na nje ya nchi yanayojihusisha na mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI mkoani Mbeya yamelalamikiwa kuwa yanarudia rudia kuwapima watu ambao tayari wameshagundulika wana maambukizi ya virusi vya UKIMWI hali ambayo inasababisha takwimu za maambukizi ya virusi vya ukimwi kuonekana ziko juu kuliko uhalisia wa maambukizi hayo. 

vikundi vya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi wilayani Mbarali, maarufu kwa jina la Konga ndivyo vimetoa malalamiko hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya furaha yangu, pima, jitambue ishi ambayo inalenga kuwahamasisha wanaume wajitokeze kupima Virusi vya Ukimwi.