Back to top

MWIGULU: IDA NI DIRISHA LA MIKOPO YENYE MASHARTI NAFUU

28 April 2024
Share

Waziri wa Fedha, Dk.Mwigulu Nchemba, amesema Mfuko Maalum wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA), ni dirisha ambalo limekuwa likitoa mikopo kwa masharti nafuu, riba kwa kiwango cha chini na muda wa kurudisha umekua mrefu ambapo Tanzania kwa kiwango kikubwa imekuwa ikitumia dirisha hilo kupata fedha ambazo zimekua zikitumika katika kuendeleza sekta za huduma za jamii kama vile elimu, maji pamoja na umeme.
.
Mhe.Mwigulu ameyasema hayo, wakati akizungumza kwenye mkutano maalumu wa Mfuko huo, wa kujadili vipaumbele vya Afrika, ili viweze kuzingatiwa katika maandalizi ya Mzunguko wa 21, unaotarajiwa kuanza Julai 2025 – Juni 2028.
.
Amesema, riba ya mikopo ya mfuko huo haizidi 2% na umekuwa ukitoa mikopo yenye masharti nafuu kwa nchi za Afrika, ili kuzipunguzia nchi hizo kupata mikopo kutoka benki za kibiashara ambayo huwa na gharama kubwa.