Back to top

WAKANDARASI WASIMAMIWE ILI WAFANYE KAZI KWA UFANISI

28 April 2024
Share

Waziri wa Ujenzi, Mhe.Innocent Bashungwa, amemuagiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Eng. Mohamed Besta, kuhakikisha anawasimamia kikamilifu Wakandarasi wote waliopewa kazi ya kurejesha miundombinu iliyoathiriwa na mvua, ili wafanye kazi kwa ufanisi.
.
Bashungwa ametoa agizo hilo wakati akikagua zoezi la urejeshaji wa miundombinu ya barabara kuu ya Pwani - Lindi katika eneo la Kimanzichana Kusini, lililoathiriwa na mvua na kusababisha barabara hiyo kufungwa kwa muda.
.
Pia Waziri huyo amewataka mameneja wa TANROADS mikoa yote kuendelea kufanya ukaguzi wa madaraja, makalavati pamoja na kuondoa matope na takataka, huku akiagiza zoezi liwe endelevu.