Rais Magufuli amteua Ludovick Utouh kuwa Mwenyekiti wa TEITI


Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Ludovick S.L Utouh kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative - TEITI).

Uteuzi wa Bw. Utouh unaanza leo tarehe 20 Juni, 2018.