Back to top

UCHAGUZI JIMBO LA KWAHANI KUFANYIKA JUNI 08, 2024

02 May 2024
Share

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kwahani, lililopo katika Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, visiwani Zanzibar.
.
Uchaguzi huo, ambao unatarajiwa kufanyika Juni 08, 2024, umetangazwa baada ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akimtaarifu Mwenyekiti wa Tume hiyo kuhusu uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Kwahani.
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Tume hiyo imeeleza kuwa fomu za uteuzi wa Wagombea zitaanza kutolewa Mei 17, 2024 hadi Mei 23, 2024, huku kampeni za uchaguzi huo zikitarajiwa kuanza Mei 24, 2024 hadi Juni 07, 2024.