Sanamu kubwa ya mwanajeshi aliyeshika bunduki katika makumbusho ya mashujaa wa vita vya majimaji iliyojengwa kwa ajili ya kuwaenzi wanajeshi waliopigana vita vya Kagera imekuwa kivutio kikubwa cha utalii mkoani Ruvuma.
Akizungumza na ITV Muhifadhi kiongozi wa makubusho ya vita vya maji maji Bw. Baltazari Nyamusya amesema sanamu hiyo ina mafundisho makubwa chini yake ikiwa na maandishi yanayosomeka sisi mababu zenu mashujaa wa majimaji tumetoa maisha yetu kutetea taifa letu,tumetimiza wajibu wetu uliobaki ni wenu.