Shule ya msingi Emaco Geita yafungwa kwa wiki moja.

Mkurugenzi wa shule ya msingi Emaco Vision English Medium Cosmas Kibela amesema uongozi umeamua kuifunga shule hiyo kwa wiki moja ambapo pia umepanga kununua vifaa maalum vya kuzuia radi.

Kutokana na hatua hiyo pia wanafunzi 20 wameruhusiwa kutoka hospitali kati ya 23 waliojeruhiwa katika mvua kubwa iliyoambatana na radi kunyesha jana mjini geita na kusababisha vifo vya watoto sita.