Kamishna wa idara ya uhamiaji nchini Kamishna Jenerali Dkt. Anna Makakala ametembelea kituo cha uhamiaji cha Congresso mkoani Lichinga nchini Msumbiji na kusema ushirikiano baina ya maafisa uhamiaji wa Msumbiji na Tanzania utasaidia kuondoa changamoto ya wahamiaji haramu.
Akizungumza na maofisa uhamiaji wa Msumbiji Kamishna wa uhamiaji Generali Dkt. Anna Makakala amesema kuwa ushirikiano wa idara ya uhamiaji ya Tanzania na Msumbiji utasaidia kudhibiti wahamiaji haramu wanaotumia kuvuka maeneo yasiyo rasmi maarufu kama vipenyo.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi.Christina Mndeme amebainisha changamoto katika idara ya uhamiaji mkoani humo ikiwemo ubovu wa magari.
Mbali na kutembelea nchini Msumbiji katika ziara yake mkoani Ruvuma Kamishna Jenerali wa uhamiaji Dkt. Makakala ametembelea vituo vya uhamiaji vya Tunduru,Ruvuma,Mbinga na Mkenda mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.