Back to top

JKT WAANZA KUACHANA NA MATUMIZI YA KUNI

05 May 2024
Share

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limeanza kuachana na matumizi ya kuni kwa ajili ya kupikia na badala yake limeanza kutumia nishati safi ya kupikia, katika vikosi vyake vilivyopo maeneo mbalimbali nchini, hali ambayo imeelezwa kuwa itasaidia kuzuia ukataji miti hovyo.
.
Matumizi hayo ya nishati safi ya kupikia, yameanza ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa agizo la serikali kwa Taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 kwa siku, kuachana na matumizi ya kuni kwa lengo la kutunza mazingira.


Akizungumza na ITV wakati wa uzinduzi wa nishati hiyo katika Kikosi cha Jeshi cha 825 Mtabila, kilichopo Kasulu mkoani Kigoma, Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena, amesema Jeshi hilo ni wadau wakubwa katika kuhakikisha mazingira yanakuwa salama na katika kuhakikisha hilo linafanikiwa wameacha kukata miti na badala yake wamekuja na kampeni ya kupanda miti katika maeneo yote ya vikosi vya Jeshi hilo.