Wagonjwa wa Corona Kenya wafikia 50.

Idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona nchini Kenya imeongezeka na kufikia 50,hii ni baada ya watu wengine 8 kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo katika muda wa saa 24 zilizopita.

Maambukizi hayo mapya yakiwa ni ya Mkenya mmoja ambaye yuko karantini na wengine 7 waliochangamana na wagonjwa wa hapo awali.
]
Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema kuwa Nairobi inaongeza kwenye maambukizi hayo kwa wagonjwa 34,Mombasa 3,Kilifi 6,Kajiado 3,Kwale 3 na Kaunti ya kitui 1.