Independent Television Ltd
Wanne wafa wakiwemo madereva baada ya malori kugongana uso kwa uso wilayani Mvomero.

Watu wanne wamefariki dunia papo hapo wakiwemo madereva wawili baada ya kutokea kwa ajali mbaya iliyohusisha kugongana uso kwa uso kwa malori ya mizigo katika eneo la sangasanga wilayani mvomero, barabara kuu ya Morogoro-Iringa.

ITV imefika eneo la tukio na kukuta jitihada za kunasua miili ya watu wote wanne waliokuwa katika malori hayo  zikiendelea kufanywa na askari polisi, zimamoto na wasamaria wema, ukiwemo mwili wa dereva wa fuso iliyokuwa imebeba viazi kutoka uelekeo wa Iringa kuelekea Morogoro, utingo wa gari hiyo na abiria mmoja mwanamke ambao hawajatambulika mara moja pamoja na dereva wa lori semi tela aina ya man, mali ya kampuni ya Greenwhich Enterprises inayoelezwa kuwa ni kampuni tanzu ya mohamed enteprises iliyokuwa na shehena ya mafuta ya kula ikitokea dar es salaam aliyetambuliwa kuwa ni Almas Halfan.
 
Katika eneo la ajali gari aina ya fuso imeonekana kuhama upande wake wa barabara na kulifuata semi tela upande wake na kugongana uso kwa uso na kuharibika vibaya hasa sehemu za mbele huku injini ya fuso ikirushwa pembeni  baada ya kung'oka kutoka kwenye gari ambapo mashuhuda wakazungumzia ajali hiyo.
 
Wakizungumza eneo la tukio,mkuu wa polisi wilaya ya Mvomero Julius Lukindo, amesema bado wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha ajali na kuwataka madeva kuwa makini kwa kuzingatia sheria za barabarani huku kamanda wa jeshi la zimamoto mkoa wa Morogoro ramadhan pilipili akazungumzia hatua walizochukua baada ya ajali hiyo.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather