Independent Television Ltd
CUF yaiomba TAKUKURU kuchunguza kiasi cha shilingi milioni 369 fedha za ruzuku za chama.

 Chama cha wananchi-CUF-kimeiomba taasisi ya kuzuia na kupambana rushwa-TAKUKURU- kuingilia kati kuchunguza kiasi cha shilingi milioni 369 fedha za ruzuku za chama zilizokwemo katika akaunti ya chama kuchukuliwa na watu wasiojulikana baada ya kuzuiliwana na msajili wa vyama vya siasa kutokana na mgogoro unaoendelea ndani ya chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti wa muda wa chama cha CUF Bwana Julius Mtatilo amesema kiasi hicho cha fedha kilikuwa ni sehemu ya shilingi milioni 600 za chama zilizotokana na ruzuku ya chama ambapo amesema mbaka sasa chama hicho kimeamua kusitisha mkutano wa bodi ya wadhamini, kamati kuu na wanasheria wa chama ili kufanya usahihi kutokana na tukio hilo.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather