Independent Television Ltd
Rais Magufuli afungua barabara ya Lamadi –Bariadi mkoani Simiyu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk John Pombe Magufuli amewasili mkoani Simiyu kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo leo mchana aweka jiwe la msingi la ujenzi wa  hospitali ya mkoa wa Simiyu na baadaye kufungua barabara ya Lamadi–Bariadi yenye urefu wa KM 72.8 iliyojengwa na kampuni ya CCCC ya China.

Mapema akiongea na wananchi wa kijiji cha Masanza wilayani Busega amesema serikali imejipanga kuhakikisha inawatumikia watanzania na kuwaomba wananchi waiamini serikali huku akisisitiza kauli yake ya kufanya kazi na kwamba hakitakuwepo chakula cha msaada wananchi lazima walime mazao yanayostahimili ukame.
 
Aidha Rais amewahakikishia wananchi wa Busega kuwa tatizo la maji walilonalo serikali italishughulikia na kuahidi kumtuma Waziri wa maji ili aweze kuja kuangalia tatizo hilo.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather