Independent Television Ltd
Mkuu wa wilaya ya Kibondo aagiza wazazi wote wasiowapeleka watoto shule kufikishwa mahakamani.

Mkuu wa wilaya ya Kibondo Luis Bura ameagiza wazazi wote ambao hawatawapeleka watoto kuanza darasa la kwanza na elimu ya awali mwaka huu kukamatwa na kupelekwa mahakamani baada ya kubainika kuwa hadi sasa ni asilimia 23 tu ya watoto wanaostahili ndio wameandikishwa.

Mkuu huyo wa wilaya ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, ameeleza hayo wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa Kiwilaya katika kijiji cha Busunzu, ambapo amesema serikali haitavumilia wazazi wenye tabia ya kutowapeleka watoto shule na kuanzia mwezi ujao msako mkali utafanywa kila nyumba kubaini watoto ambao hawajaandikishwa.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kibondo Juma Mnwele amesema bado wilaya hiyo haijajitosheleza kimiundombinu katika shule za msingi kukiwa na upungufu wa vyumba 132 vya madarasa huku baadhi ya wazazi wanawake wakiwalaumu waume zao kutojali kuwapeleka shule watoto.

Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather