Independent Television Ltd
Waziri Mkuu aziagiza halmashauri zenye wafugaji wenye makundi makubwa ya mifugo kufuga kisasa.

Waziri mkuu Mh Kassimu Majaaliwa ameziagiza na kutoa maelekezo kwa halmashauri zenye wafugaji wa mifugo kuanza mara moja hatua ya kubadilisha mfumo wa ufugaji  kutoka  kuchunga makundi makubwa ya mifugo yasiyokuwa na ubora sambamba na kufanya sensa na kupunguza idadi ya mifugo badala yake kuanza kuwaelimisha wazee wa jamii ya wafugaji kubadilika kifikra ili wafuge kwa njia ya kisasa ili kuepusha migogoro ya ardhi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo kwenye kikao na watendaji wa serikali wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro na mkoa wa Manyara pamoja na mamia ya wananchi mjini Orkesumet huku akisisitiza kwamba bado walio wengi hufuga makundi makubwa yasiyo na ubora hasa kwenye ngozi na nyama na sasa mipango ya serikali ni kufuga kwa tija na kupandisha  thamani ya nyama nje ya nchi.
 
Hata hivyo baadhi ya wafugaji wakizungumzia agizo hilo la serikali wamekiri hasa kutokana na ukame uliosababisha kufa kwa mifugo mingi lakini kikubwa wakihitaji elimu hususani kwa wazee wa mila maarufu kama Malaigwanani
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather