Independent Television Ltd
Makamu wa Rais ameviagiza vyombo vya dola kuongeza kasi ya mapambano ya dawa za kulevya.

Makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama katika mkoa wa Mwanza kuongeza kasi katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya ili kuokoa vijana ambao ni nguvu kazi kubwa ya taifa inayoendelea kuangamia kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.

Mama Samia ametoa agizo hilo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika wilaya ya Ilemela kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa maagizo yake 14 aliyoyatoa November mwaka jana ikiwemo sekta ya elimu, hifadhi ya mazingira na ujenzi wa vituo vya uchunguzi wa dalili za awali za saratani ya matiti na mlango wa kizazi, ambapo ametumia fursa hiyo kutaka vita dhidi ya dawa za kulevya iende sambamba na mapambano dhidi ya uvuvi haramu katika ziwa Victoria.
 
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan pia amezidi kukoleza moto vita dhidi ya dawa za kulevya, ambayo katika mkoa wa Mwanza imewezesha kukamatwa kwa watuhumiwa 12, akiwemo mfanyabiashara wa duka la vipuri vya magari jijini Mwanza Kassim Hemed Hamad, aliyenaswa februari 10 mwaka huu nyumbani kwake mtaa wa Kanyerere kata ya Mahina akiwa na kete 240 za heroine.
 
Makamu wa rais aliwasili jumanne wiki hii mkoani Mwanza kwa shughuli ya ufunguzi wa kongamano la utafiti wa kisayansi la bonde la ziwa Victoria lililohudhuriwa na zaidi ya washiriki 500 kutoka nchi za Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya na Tanzania. Bonde la ziwa Victoria lilitengwa na jumuiya ya Afrika Mashariki kama eneo maalum la pamoja lenye maslahi ya ukuaji wa kiuchumi.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather