Independent Television Ltd
Viongozi 6 wa chama kikuu cha ushirika cha Songea na Namtumbo wamekamatwa kwa ubadhirifu wa bilioni 1.

Tume iliyoundwa kuchunguza ubadhirifu kwenye   chama  kikuu cha ushirika cha Songea na Namtumbo(SONAMCU) imebaini ubadhirifu wa shilingi bilioni moja ambapo kutokana na ubadhirifu huo aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya SONAMCU Bw. Philoteus Mbawala anashikiliwa na polisi na viongozi wengine watano kwa tuhuma za ubadhirifu huo.

Mkurugenzi msaidizi wa rasilimali  watu wa tume ya maendeleo ya ushirika nchini  bw. Kawina Kawina  amesema kuwa watu wengine waliotajwa kwenye ripoti hiyo    wanaoshikiliwa  polisi kwa  tuhuma za kuhusika  na ubadhirifu wa shilingi bilioni moja  ni Hatibu lihonda,Damas Ngonyani,Awadhi Nyoni na Eva Kihwili.
 
Mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Pololeti Kamando Mgema amesema kuwa wataendelea kuondoa mchwa wa ushirika ili ushirika mkoani Ruvuma  ukae sawa.
 
Mbunge wa jimbo la Namtumbo ambaye ni mdau wa ushirika mhandisi Edwini  Ngonyani amewataka viongozi wa SONAMCU kutafuta ufumbuzi wa malamiko ya fedha za wakulima  ili wakulima walipwe fedha zao wanazodai.
 
Hivi karibuni bodi ya chama kikuu cha ushirika cha Songea na Namtumbo(SONAMCU) ilivunjwa na kuundwa upya kutokana na kukiuka sheria za ushirika.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather