Independent Television Ltd
Bunge lasitisha vikao vyake ili kuuaga mwili wa Marehemu Elly Macha.

Bunge la Tanzania leo limesitisha shughuli zake ili kuweza kutoa fursa kwa waheshimiwa wabunge waweze kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, Chadema Dkt. Elly Macha aliyefariki dunia katika hospitali ya New Cross, nchini Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu.

Katika kile kilichoonekana kuwa  ratiba za kawaida za bunge zisiharibike Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai alieleza wabunge jana kuwa bajeti ya TAMISEMI na ile ya Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora majadiliano yalitakiwa yamalizike jana hiyo hiyo ili leo shughuli za kuuga mwili wa Dkt. Macha ziweze kufanyika.
 
Agizo hilo la Spika wa Bunge lilitekelezeka jana hiyohiyo ambapo bunge liliweza kuhitimisha bajeti ya ofisi hizo za rais majira ya saa tatu usiku.
 
Dkt.Macha enzi za uhai wake akiwa mbunge wa vitti maalum CHADEMA alikuwa akiwakilisha watu wenye ulemavu Bungeni.
 
Mwenyezi Mungu amuweke Mahala Pema Amina.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Wito wakuwataka wafugaji kujiunda kwenye vikundi kuanzisha viwanda vya kuchakata mazao ya mifugo. Je, mazingira ya masoko yameandaliwa?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather