Independent Television Ltd
Ziwa Rukwa hatarini kukauka kwa uharibifu wa Mazingira.

Serikali imeamua kulihifadhi ziwa Rukwa, kwa kuweka sheria zitakazodhibiti shughuli za kibinadamu za kilimo, ukataji misitu na ufugaji ambazo zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa kuharibu mazingira na kulifanya ziwa hilo kupungua kina kwa kasi, hadi kufikia mita tatu sasa toka mita tisa miaka ishirini iliyopita, na kuwa kwenye hatari kubwa ya kukauka kabisa.

Naibu katibu mkuu wa ofisi ya makamu wa rais Muungano na Mazingira Mhandisi Ngosi Mwihava, akimwakilisha waziri wake katika kuuzindua mradi mkubwa wa hifadhi ya mazingira, wa jumuiko la pamoja na suluhisho la pamoja wa jupasupa, unaotekelezwa na shirika la mazingira mkoani Rukwa la Kaeso na wadau mbalimbali, kwenye mikoa ya Rukwa na Katavi kwa ufadhili wa zaidi ya shilingi bilioni 2.5, kutoka kwa shirika la kimataifa la uhifadhi asilia la nchi ya Uholanzi la IUCN, amesema sheria hiyo ipo katika hatua mbalimbali kabla ya kutangazwa gazetini.
 
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa shirika hilo la kaeso Bw. Ozem Chapita, amesema mikoa ya rukwa na katavi inayotoa mchango mkubwa katika uzalishaji wa mazao ya chakula nchini, inakabiliwa na uharibifu mkubwa wa mazingira, hali inayotishia kupotea kwa mito mbalimbali ukiwemo mto katuma inayomwaga maji katika ziwa Rukwa, na kufanya kusiwepo na mvua za uhakika hivi sasa.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather