Independent Television Ltd
Kampuni iliyokamatwa na kemikali bashirifu kupelekwa mahakamani.

Sakata la  Kampuni ya Techno Net Scientific LTD la kukutwa na kemikali bashirifu  bila ya kibali limechukua sura nyingine baada ya Mkemi Mkuu wa serikali kusema kampuni hiyo itapelekwa mahakamni kwa kufanya shughuli zake kinyume na taratibu.

Akizungumza Ofisi kwake Mkemia Mkuu wa serikali Profesa Samwel Manyere amesema uchunguzi umeanza na muda wowote ukikamilika kampuni hiyo itafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao.
 
Aidha Mkemia huyo ameitahadharisha jamii kutojishughulisha na kemikali  bila ya kuwa na vibali kwani ni hatari kubwa na wawafichue wanaofanya hivyo. 
 
Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za kampuni ya Techno Net Scientific LTD inaojishughulisha na  uingizaji na uuzaji wa kemikali  nchini zikiwemo kemikali bashirifu zilizokamatwa eneo loa Mwenge .
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Wakulima kulazimishwa kuuza korosho kinyume na bei elekezi. Je ni utawala bora?
Ndio
Hapana
Vote Now
Results
Weather