Independent Television Ltd
Mgogoro wa kugombea ardhi wasababisha wanawake na watoto kukosa makazi Monduli.

Mgogoro wa kugombea ardhi uliokuwa unafukuta katika kijiji cha Kilimatinde kilichoko kata ya Moita wilayani  Monduli mkoani Arusha umesababisha nyumba zaidi ya saba kubomolewa na watu zaidi 50 kulala nje kwa siku tatu  sasa jambo linalohatarisha maisha yao na hali ni mbaya zaidi kwa wananwake na watoto.

ITV imefika katika kijiji hicho na kushuhudia wanawake na watoto wakihangaika kutafuta msaada ukiwemo wa  kujisitiri wao na watoto wao huku wakiangua vilio vya kuomba msaada.
 
Mmoja wa wamliki wa nyumba zilizoboloewa Bwana LEPILALI LUKASI pamoja na kukiri kuwepo kwa mgogoro wa muda  mrefu amesema hatua ya kuvunja makazi yao na ni ukiukwaji wa sheria na haki za binadamu.
 
Mtendaji wa kata ya Moita Bwana EMANUEL NAISIITIE amekiri kuwa kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu wa kugombea eneo hilo kati ya wananchi hao na mwekezaji na kwamba anaendelea kufuatilia kujua kilichotokea.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather