Independent Television Ltd
Urusi kuwafukuza maofisa wa ubalozi wa Marekani na kufunga majengo yake nchini humo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imeonya kuwa itawafukuza maofisa wa ubalozi wa Marekani na kuyafunga baadhi ya majengo ya Marekani nchini Urusi kama Marekani itaendelea kuzifunga nyumba za makazi zinazotumiwa na maofisa wa Urusi nchini humo.

 Katika kulipiza kisasi kuhusu madai kuwa Urusi iliingilia kati kwa kudukua hati nyeti katika serikali ya Marekani katika  uchaguzi mwaka jana, Marekani iliwafukuza wanadiplomasia 35 wa Urusi na kuzifunga baadhi ya nyumba zilizokuwa zikikaliwa na wanadiplomasia hao.
 
Katika mazungumzo yao juma lililopita, marais wa Marekani na Urusi pamoja na kuzungumzia suala hilo, hawakufikia muafaka.
 
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya NJe ya Urusi MARIA ZAKHAROVA ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa Urusi italazimika kuchukua hatua za kulipa kisasi kama Marekani haitazifungua nyumba hizo.
 
Naibu Waziri wa Mambo ya NJe wa Urusi Bwana SERGEI RYABKOV na mwenzake wa Marekani TOM SHANNON wanatarajiwa kukutana keshokutwa ili kulijadili upa  suala hilo.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather