Independent Television Ltd
Zaidi ya shilingi Milioni 168 za ushuru wa magari yanayovuka mpaka wa Tunduma hazijulikani zilipo.

Zaidi ya shilingi milioni 168 ambazo zimekusanywa na watumishi wa halmashauri ya mji wa Tunduma kama ushuru wa magari yanayovuka mpaka wa tunduma kwenda nje ya nchi hazijulikani zilipo, huku halmashauri hiyo pia ikipata hasara ya zaidi ya shilingi bilioni mbili kutokana na watumishi wake kushindwa kukusanya ushuru kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara mjini Tunduma, Mbunge wa jimbo la Tunduma, Mhe.Frank Mwakajoka amesema ametembelea mpaka wa Tunduma kwa lengo la kukagua mapato ya halmashauri ya mji wa Tunduma na kubaini upotevu wa zaidi ya shilingi milioni 168 ambazo ni ushuru wa halmashauri kwenye chanzo cha mapato cha Custom.
 
Katika hatua nyingine,Mbunge Mwakajoka amesema wananchi waliojenga jirani na mpaka wa Tanzania na Zambia, ambao wameamuliwa na waziri mkuu kubomoa nyumba zao, walipewa maeneo hayo kihalali na serikali na  wanazo hatimiliki za ardhi hiyo, hivyo kama serikali imeamua kuwaondoa wanapaswa kulipwa fidia na kupewa maeneo mengine ya kujenga kabla hawajaondolewa.
 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Tunduma, Mhe.Ally Mwafongo ametangaza kuondoa ushirikiano baina mkuu wa wilaya ya Momba na baraza madiwani la maji wa Tunduma pamoja na wenyeviti wote wa serikali za mitaa inayoongozwa na chama chake cha Chadema kwa madai kuwa mkuu huyo wa wilaya anawasumbua wananchi hasa wamachinga kwa kuamuru waondolewe kwenye maeneo yao ya biashara bila kifuata utaratibu wala kushirikisha uongozi wa halmashauri.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather