Independent Television Ltd
Serikali mkoani Singida yatoa mwezi mmoja kwa Watendaji kurejesha zaidi ya Sh.Milioni 11 fedha za chakula au kutaifishwa mali zao.

Serikali Mkoani Singida imetoa mwezi mmoja kwa watendaji ishirini na moja wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni   kurejesha Shlingi zaidi ya Milioni kumi na moja kati ya Shilingi Miloni 15 ambazo zilikuwa fedha za msaada wa mauzo ya chakula cha msaada wa njaa na watakao shindwa mali zao zitaifishwa.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dakta.REHEMA NCHIMBI ametoa agizo hilo katika Baraza maalumu la Madiwani la Halmashauri ya Manyoni ambalo limejadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.
 
Kwa upande wake Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mheshimiwa DANIEL MTUKA amesema, upatikanaji wa chakula cha njaa kutoka serikalini ni mgumu kwa sababu wanapopewa chakula na kuuziwa wananchi fedha hizo zinatakiwa kutumika kununulia chakula cha akiba,lakini baadhi ya watendaji wa Manyoni siyo waaminifu.
 
Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni limejadili hoja 78 za Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoka katika idara balimbali za halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather