Independent Television Ltd
Watu 3 wamefariki katika ajali za barabarani mbili tofauti wilayani Manyoni.

Watu watatu wamekufa katika ajili mbili tofauti wilayani Manyoni ,ikiwemo ya mbunge wa Manyoni mashariki kumgonga mwanafunzi wa darasa la kwanza na kufariki papo hapo ,na ajali nyingine gari aina ya Hiace kuligonga lori kwa nyuma na kusababisha vifo vya watu wawili papo hapo.

Akithibitisha kutokea kwa vifo hivyo kamanda wa polisi mkoani Singida  ACP Debora Magiligimba  amesema matukio hayo yametokea tarehe kumi mwenzi huu na amemtaja mbunge wa Manyoni mashariki Bwana Daniel Mtuka, aliyekuwa akiendesha gari lenye usajili wa namba T.238 DGU aina ya Prado  alimgonga mwanafunzi   Salome Paschal  wa shule ya msingi  Sukamahela   aliyekuwa akijaribu kuvuka barabara. 
 
Katika ajali  nyingine kamanda Magiligimba amesema gari aina ya toyota hiace  iligonga lori  kwa nyuma lenye usajili wa namba T.407 DES  na tela  T.809 CAS aina ya DAF na kusababisha  kifo cha dereva raia wa Kongo  ambaye hakufahamika jina na afisa elimu sekondari wilaya ya Ngara  mkoani  Kagera  Bwana  Alfred Katega .
 
Akiongea kwa simu mganga mkuu wa wilaya ya Manyoni Daktari Nelson  Bukuru amethibitisha kupokea maiti mbili za ajali ya gari aina ya hiace kulingonga lori ambazo zimepata majeraha kichani na alipotakiwa kueleza ajali ya mbunge kumgonga mwanafunzi simu yake ilikatika na haikupatikana ,ITV haikuishia hapo ilimtafuta mbunge na simu yake ilipokelewa na mtu mwingine na kusema kuwa yupo kwenye kikao . 
Ajali zote hizo mbili ambazo zimesababisha vifo vya watu watatu  wilayani Manyoni kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Singida amesema zimesababishwa na uzembe wa madereva wa gari  aina ya Hiace na Prado.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather