Independent Television Ltd
Naibu Waziri Mhe.Mavunde awaka waajiri wote kuhakisha kuwa wanazingatia sheria na kanuni za ajira

Naibu waziri vijana, kazi na ajira Mhe.Anthony  Mavunde amewaka  waajiri  wote kuhakisha  kuwa wanazingatia  sheria na kanuni za  ajira  na kama itabanika  uwepo wa wajiri ambao hawatafuata sheria na kanuni  hizo serikali haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Mhe.Mavundeameyasema hapo mjini Dodoma wakati akizungumza na  wadau  wa usafirishaji kuhusu tuzo ya usafirishaji na kuhimiza  ajira  salama  ili kuepush ajali za mara kwa mara.
 
Naye mshindi wa kwanza wa tuzo  zinazotolewa na  mamlaka ya udhibiti  wa   usafiri  wa  majini na nchi kavu  SUMATRA Bw. Melei  Shabiby   Mkurugenzi  msaidizi wa kampuni ya Shabiby amesema   wanashukuru  namna SUMATRA  inavyofanya kazi  na sekta hiyo.
 
Bw. Edward  Magawa ni  mmoja  ya wadau wa usafirishaji ambaye   anasema kwa kushirikiana  na jeshi  la  polisi  na wadau  wengine  kila mara  sekta ya usafirishaji  imezidi  kuimarika  japo zipo changamoto mbalimbali barabarani kama ubovu wa barabara.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather