Independent Television Ltd
Jeshi la polisi Dodoma limesema halitavumilia udhalilishaji wa kidini wa namna yoyote ile.

Jeshi la polisi mkoani Dodoma limewaonya viongozi wa dini mkoani humo ambao  wana tabia ya kufanya vitendo ambavyo ni kinyume na mafundisho  ya dini na kuwataka viongozi wa dini kuwafichua wanaofanya vitu vya namna hiyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa huo Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa polisi Gilles Murroto amewaambia viongozi wa dini kuwa hawezi kuvumilia vitendo vya namna  hiyo kuendelea.
 
Kamanda Murroto amesema kutokana na utandawazi ulivyo hivi sasa kuna vingi vinafanyika na vimekuwa na madhara kwa jamii hivyo Jeshi la polisi halitavumilia udhalilishaji wa kidini wa namna yoyote ile.
 
Katika mkutano huo baina ya kamanda wa polisi wa mkoa wa Dodoma na viongozi wa dini,viongozi hao wamemhakikisha Kamanda Murroto kuwa watakuwa vinara wa kufichua vitendo hivyo.
 
Kamanda Murroto amewaagiza viongozi wa dini kuhakikisha nyumba za ibada wanazoziongoza zinakuwa na ulinzi wa uhakika.
 
Pia  amewaambia viongozi wa dini mkoani humo kuwa ukosefu wa ulinzi katika nyumba za ibada kwa namna moja ama nyingine imekuwa ni kishawishi kwa watu wenye nia ovu kufanya vitendo hivyo vya uhalifu.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather