Independent Television Ltd
Kampuni ya vinywaji ya Cocacola imezindua kipindi cha Coke Studio.

 Kampuni ya vinywaji baridi ya Cocacola imezindua kipindi cha kusisimua cha muziki kitakachojulikana kama Coke Studio Afrika ambacho kitawahusisha wanamuziki wa miondoko ya aina tofauti kutoka nchi mbalimbali barani Afrika ili kupata mchanyato wa kisasa wenye asili ya Afrika.

Kipindi hicho ambacho kitakuwa kinarushwa hewani katika mchi ya Kenya, Uganda, Nigeria na Tanzania kupitia kituo chako cha ITV kitakuwa kinaonekana kwa vipindi nane kwa dakika 45 kila kimoja pamoja na masaa mawili ya kipindi maalum cha mwaka mpya kwa kujumuisha vipaji mbalimbali vya wanamuziki nguli kutoka bara la Afrika.

Msimu wa kwanza wa kipindi hicho utawahusisha wasanii nyota ambao kutoka Tanzania ni Diamond platnumz, Lady Jay dee na kundi la muziki wa taarab asilia la Culture music kutoka Zanzibar wengine ni Salif Keita kutoka Mali , Jimmy Jatt nabez kutoka Nigeria, miss Karun na Just a band kutoka Kenya, hip hop panstula kutoka Uganda na wengineo ambapo meneja bidhaa wa Cocacola Morrice njowoka amesema kipindi hicho kinatoa fursa kwa wanamuziki kujitangaza na kupanua soko la muziki wao.

Jumla ya wasanii 24 kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wameshirikiana kutengeneza muziki mpya wenye mchanganyiko wa vionjo vya kisasa vyenye asili ya Afrika ambapo mwanamuziki Chege Chigunda kutoka kundi la wanaume famili amesema endapo wanamuziki wa Tanzania wataitumia fursa hiyo vizuri watafikia malengo waliyojiwekea.

Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Wakulima kulazimishwa kuuza korosho kinyume na bei elekezi. Je ni utawala bora?
Ndio
Hapana
Vote Now
Results
Weather