Independent Television Ltd
Mashindano ya mchezo wa mieleka ya ridhaa ya kuwania kombe la Mwal. Nyerere yameanza leo

 Mashindano ya mchezo wa mieleka ya ridhaa ya kuwania kombe la Mwalimu Nyerere yameanza leo ambapo wachezaji kutoka vilabu vinne vya jijini Dar es Salaam wamechuana vikali katika mzunguko wa kwanza uzito wa kilogramu 55 Bashiru Athumani ameibuka mshindi baada ya kumchapa Mohamed Kumwembe kwa point 3-1.

Wakati katika mchezo uliofuata Mohamed Kumwembe amemchapa William Zingira kwa point 3-1 huku Subiri Newton naye akimshinda Hassan Zaharani kwa point 5-0 na kwa upande wa uzito wa kg 74 Selly Ally naye amemchapa Benjamini Soko kwa point 5-0.

Nae mchezaji  Gervas Chilikwely nae amemchapa  Hashim Zongo kwa point 5-2 na kwa uzito kg 120 Habibu Lema amemfunga Boniface Tugala kwa point 5-0.

Mashindano hayo yamezinduliwa na naibu kamishna jenerali wa jeshi la zima moto na uokoaji Lodwino Mgumba ambaye ameahidi kulipa deni la chama cha mieleka la shilingi milioni walizokuwa wanadaiwa na shirikisho la kimatifa la mchezo wa mieleka la ridha na kusababisha chama hicho kufungiwa kushiriki katika michezo ya kimataifa kwa kipindi kirefu.

Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather