Independent Television Ltd
Sakata la baadhi ya wanachama wa Simba Kumtaka Rage ajiuzulu limeendelea..

 Sakata la baadhi ya wanachama wa Simba kumtaka mwenyekiti wao kujiuzulu limeendelea kushika kasi huku mwenyekiti huyo akikataa kujibizana na wanachama hao kwa madai anasimamia katiba ya timu hiyo.

Wasafiri muwe macho chombo chaenda mrama,mawimbi yamewakumba katikakati ya bahari na wapo wanaotoboa jahazi,hamkani si shwari.riwaya ya Simba iliyobuniwa na mwenyekiti pamoya na kamati yake ya utendaji imeendelea sehemu ya sita ambapo washiriki wengine ambao ni wanachama wameendelea kushinikiza mwenyekiti wao aachie ngazi.

Akiongea kwa njia ya simu akiwa mkoani Dodoma Ismail Aden Rage amesema hawezi kujibizana na wasiyofahamu katiba ya Simba yeye anatetea katiba ya klabu yake.kwa msigano huu ni afadhali meli iweke nanga.

Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Wakulima kulazimishwa kuuza korosho kinyume na bei elekezi. Je ni utawala bora?
Ndio
Hapana
Vote Now
Results
Weather