Independent Television Ltd
TFF imempata katibu mkuu mpya pamoja mkurugenzi wa utawala na masuala ya kisheria.

 Hatimaye shirikisho la soka nchini TFF limempata katibu mkuu mpya pamoja mkurugenzi wa utawala na masuala ya kisheria.

Aliyewahi kuwa katibu mkuu wa timu ya Yanga Sylestine Mwesigwa amerejea katika ulingo wa soka na safari hii akiingia kupitia mlango wa mbele,amefanikiwa kuwa katibu mkuu mpya wa TFF,kadhalika aliyewahi kuwa katibu mkuu wa Simba Evodienc Mtawala naye akilamba turufu ya kuwa mkurugenzi wa utawala na masuala ya sheria .

Kwa upande wa pili wa turufu rais wa TFF Gama Malinzi ameshtushwa na taarifa za kuuguwa ghafla kwa mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga na Taifa stars Edibil Jons Lunyamila na kuiomba jamii ya wanamichezo na serikali kumsaidia mchezaji huyo kwa imam.

Lunyamila mshambulizi wa pembeni aliye na kasi na chenga za fadhaa amelazwa hospitali ya Mwananyamala akiwa dhohoful-twakuombea upate salama. 

Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather