Back to top

UKAME: MALAWI YATANGAZA HALI YA MAAFA

27 March 2024
Share

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera, amesema serikali yake imetangaza hali ya maafa kutokana na ukame katika Wilaya 23 kati ya 28, huku akisema nchi hiyo yenye watu milioni 20 inahitaji karibu tani laki 6 za msaada wa chakula, na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kufikisha misaada haraka.

Rais Chakwera amesema ,nchi yake inahitaji zaidi ya dola milioni mia mbili za msaada wa kibinadamu, chini ya mwezi mmoja.

Amesema ametembelea maeneo mbali mbali ya nchi yake ili kubaini ukubwa wa janga la ukame, na tathmini ya awali ya serikali imegundua kuwa takribani asilimia 40 ya zao la mahindi  limepotea na kaya milioni mbili zimeathiriwa moja kwa moja.