Back to top

“Ulanzi na Mbege” sasa kupimwa viwango na TBS

05 December 2019
Share

Shirika la viwango Tanzania (TBS) limesema linaandaa viwango kwenye pombe za kienyeji zikiwemo Ulanzi na Mbege ili pombe hizo zisilete madhara kwa watumiaji kutokana na wakati mwingine kuleta madhara kwa watumiaji yanayotokana na maandalizi mabovu  na kutothibitishwa na TBS.
  
Hayo yamebainishwa na  mkuu wa kitengo cha mahusiano cha cha TBS Bi.Roida Anduusamile wakati akitoa mafunzo  mjini Mbinga kwa wauzaji wa pombe za kienyeji,wafanyabiashara na wajasiriamli kuhusiana kuweka viwango vya TBS kwenye bidhaa zao.
 
ITV imetembelea  kwenye kilabu cha pombe za kienyeji cha wilayani Mbinga na kujionea hali ya pombe hizo na  huku wauzaji wa pombe hizo kutoka kikundi cha Maseja  wakiomba mtaji waweze kuweka pombe yao kwenye vifungashio vya makopo na kwamba nao wao wanahitaji pombe zao ziwekwe viwango vya TBS.

Mkuu wa wilaya ya Mbinga Bw.Cosmas Nsheye anasema kuwa serikali itatoa mikopo kwenye vikundi vyenye wenye viwanda kikiwemo kikundi cha kutengeneza pombe za kienyeji cha Maseja cha wilayani Mbinga.