Back to top

News

#HABARI: Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa, ametumia jukwaa la Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Uvuvi wa Bahari na Maji ya Ndani, kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, Karibiani na Pasifiki kuainisha fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye Sekta ya Uvuvi nchini na kwamba Tanzania ina rasilimali kubwa za maji ikiwa ni pamoja na bahari ya Hindi, maziwa, mito, mabwawa ya asili na ya kutengenezwa.