Back to top

13 matatani kwa tuhuma za mauaji Kahama.

10 July 2020
Share

Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linawashikilia watu 13 wanadaiwa kuhusika na tukio la mauaji ya watu  wanne na kupora mali katika kiwanda cha kuchenjulia dhahabu cha Dakires kilichopo katika mgodi mdogo wa  Namba 4 Wisolele katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama.

Akizungumzia hatua hiyo Mkuu wa oparesheni Maalum za Jeshi la Polisi SACP, Mihayo Mshikhela amesema jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata wahalifu wote waliohusika na tukio hilo pamoja na mali zilizoporwa baada ya mauaji ikiwemo cabon inayonasa dhahabu kg 385.34,bunduki aina ya short gun yenye risasi mbili ,pikipiki tano na panga moja silaha ambazo zinavyosadikiwa kutumika katika tukio la mauaji hayo.