Back to top

ADAIWA KUMUUA MUMEWE KWA KUMNG'ATA SEHEMU ZA SIRI

02 April 2024
Share

Julius Rubambi (38), ambaye ni Ofisa wa Kilimo katika Kata ya Neruma wilayani Bunda mkoani Mara, amefariki dunia baada ya kuchomwa kisu pamoja na kung'atwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo sehemu za siri, na mkewe aitwaye Elizabeth Stephen (30), ambaye naye amejeruhiwa vibaya hali iliyosababishwa alazwe katika hospitali ya Kibara, baada ya kutokea kwa ugomvi wa kifamilia kati yao.
.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Salim Morcase pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt.Vicent Naano, wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba tayari mwanamke huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi huku uchunguzi ukiendelea.