Back to top

Amuua mama yake mzazi kwa kumkata shingoni ili kuongeza utajiri.

20 February 2021
Share

Jeshi la polisi mkoani Kagera linamshikilia Fredius  Philibart Kibengo mkazi wa Omurushaka wilayani Karagwe kwa tuhuma za kumuua mama yeke mzazi kwa kumkata shingoni  kwa  kutumia kitu chenye ncha kali baada ya mganga wa kienyeji kumtaka  kupeleka damu ya mama yake. au ndugu yake wa karibu ili kutengenezewa dawa za  kuongeza utajiri kwenye biashara.
.
Katika uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi mkoani Kagera umebaini  kuwa katika kipindi cha siku chache kabla ya tukio hilo kutokea  mtuhumiwa alisafiri kuelekea nchini Burundi kutafuta dawa  za kuongeza utajiri na aliporejea nyumbani kwake alimshirikisha mkewe kuhusu mashariti aliyopewa na waganga wa kienyeji lakini mke wake hakukubaliana na masharti hayo.

Hata hivyo Februari 17 mwaka huu mtuhumiwa alionekana maeneo ya nyumbani kwa mama yake mzazi na ilipofika usiku wa kuamkia Februari 18  alimvamia mama  yake na kumkata na kitu chenye ncha kali kisha kupoteza maisha.
.
Hata hivyo kamanda malimi   amewataka wakazi wa mkoa wa kagera kujiepusha na imani za kishirikina ambazo zimekuwa zikichangia mauwaji ya wananchi wasio na hatia.