Back to top

AMUUA MKEWE, KICHWA APELEKA KWA JAMES

18 September 2023
Share

Mwanaume (27) aliyetambulika kwa jina la Vincent Bwayo amejisalimisha mwenyewe, katika kituo cha Polisi wilayani Namisindwa Mashariki mwa Uganda, baada ya kumuua kwa kumkata kichwa mkewe akimtuhumu kuchepuka, kisha kichwa kukipeleka nyumbani kwa anayemtuhumu kuchekupa na mkewe.

Naibu Mkuu wa wilaya Julie Namara, amethibitisha tukio hilo huku akisema Mtuhumiwa alifanya tukio hilo, wakati wakiwa njiani kumpeleka mkewe kwa mwanaume anayemtuhumu kuwa nae kwenye mahusiano ndipo akamvamia mkewe na kumkata kichwa.

Baadhi ya majirani wamesema walisikia mwanaume huyo mwenye watoto wanne akiongea kwa sauti kubwa kumtuhumu mkewe kuwa na mahusiano na mwanaume mwingine wa jirani aliyeitwa James Musoba.