
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limetoa taarifa juu ya kifo cha mwanafunzi aliyejulikana kwa jina la Evance Florian (17) kidato cha tatu, shule ya Sekondari Suye, ambaye amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru baada ya kushambuliwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake, kwenye ugomvi uliosababishwa na kudaiana fedha Tsh. 3000/= na kijana mmoja aliyefahamika kwa majina ya Ibrahim Shabani (18) mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha.
