
Siku moja baada ya kusambaa mtandaoni kwa tukio la mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Benson Shila (31) akiwa kwenye maporomoko ya maji ya mto Morogoro eneo la mlimani Nguzo na mtoto wake mdogo wa kiume wakiwa watupu majira ya jioni huku akiwa na panga na msumeno na kuzua hofu kwa wananchi jeshi la polisi mkoani Morogoro limesema tayari limemtia mbaroni mtuhumiwa huyo na linaendelea na uchunguzi ikiwemo uchunguzi wa kiakili.
Kamanda polisi mkoa wa Morogoro SACP Wilbroad Mutafungwa amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa baada ya polisi kupata taarifa za raia wema ambapo jitihada za askari zilifanikisha kumuokoa mtoto huyo.