Back to top

Baba mbaroni baada ya mtoto kumuua mama yake.

15 October 2021
Share

Veondre Avery (22) mkazi wa Florida amekamatwa na kushtakiwa kumuua mpenzi wake baada ya mtoto wao wa miaka miwili kufanya mauji hayo mwezi Agosti.

Polisi wanasema mtoto huyo alichukua silaha hiyo, akasogea nyuma ya mama yake na kumpiga risasi mara moja mama yake Shamaya Lynn ambaye alikuwa katika kikao cha kikazi cha mfumo wa video.

Bwana Avery mwenye umri wa miaka 22, anashitakiwa kwa mauji na kushindwa kutunza silaha hiyo.

Rekodi za mahakama zinaonesha mpaka sasa hana wakili na hajaingia katika utetezi.