Back to top

BANDARI DAR ES SALAAM YAIPITA YA MOMBASA

24 May 2023
Share

Kupitia ripoti ya Bandari zenye ufanisi zaidi duniani, Benki ya Dunia imesema kuwa Bandari ya Dar es Salaam iliyopo nchini Tanzania imeipita Bandari ya Mombasa ya Nchini Kenya, hali ambayo imetajwa kuwa tishio kwa uchumi wa Kenya.
.
Ripoti hiyo ya Utendaji wa Bandari ya Makontena ya mwaka (CPPI) 2022, imeonyesha kuwa Bandari ya Mombasa imeshika nafasi ya 326, huku Bandari ya Dar es Salaam ikishika nafasi ya 312, kati ya Bandari 348 zilizotumika katika utafiti huo, ikiwa ni tofauti ripoti hiyo ya mwaka 2021 ampao Mombasa ilikuwa nafasi ya 296 na Dar es Salaam ikiwa ya 316.
.
Bandari zingine zilizowekwa kwenye ripoti hiyo ni bandari ya Djibouti ya nchini Ethiopia, ikiwa nafasi ya 26 na bandari ya Berbera ya nchini Somalia ikiwa nafasi ya 144.