Back to top

BARABARA YA DAR, LINDI NA MTWARA SASA INAPITIKA

11 May 2024
Share

Barabara ya Dar es Salam, Lindi na Mtwara sasa imerejea katika hali yake na inapitika baada ya kukamilika urejeshaji wa mawasiliano katika maeneo yote yaliyokuwa yamekatika kufuatia uharibifu mkubwa uliosababishwa na mvua zilizoambatana na Kimbunga Hidaya.

Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) wamewakumbusha wananchi, wasafiri, wasafirishaji na watumiaji wengine wa barabara kusafiri kwa tahadhari, haswa wakati huu wa mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali.

Tarehe 9 Mei 2024  Magari ya Mizigo, Mabasi na magari mengine madogo yaliyokwama yalianza kuruhusiwa kuendelea na safari zao.