Back to top

Biteko atishia kuufunga mgodi wa Kinyambwiga.

28 December 2021
Share

Waziri wa Madini Mh. Dotto Biteko ametoa siku saba kwa wamiliki wa mashamba pamoja na wamiliki wa leseni katika mgodi wa Kinyambwiga ulipo wilayani  Bunda mkoani Mara kumaliza mgogoro wao ambao umedumu kwa zaidi ya miezi mitatu, wakigombania mashamba yanayodaiwa kuwa na dhahabu na kusisitiza kuwa endapo watashindwa kufanya hivyo ataufunga mgodi huo.