Back to top

Chanjo ya Corona ya AstraZeneca kufanyiwa majaribio kwa watoto.

21 February 2021
Share

Chuo Kikuu cha Oxford na kampuni ya dawa ya AstraZeneca imetangaza kuwa itafanya majaribio ya chanjo waliyotengeneza dhidi ya Corona (Covid-19) kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka 6-17.

Inaelezwa majaribio ya kliniki yameanza kufanywa katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Oxford St George, Hospitali ya Chuo Kikuu cha Southampton na Hospitali ya watoto ya Bristol Royal.

Katika majaribio hayo watoto 300 watahusishwa kwenye chanjo ya Covid-19 na itapewa watoto 240 katika kikundi cha majaribio, na chanjo udhibiti itapewa kwa watoto 60.

Majaribio yanalenga kupima athari za chanjo katika kuzuia maambukizi kwa watoto.

Majaribio ya kliniki ya chanjo ya Oxford-Zeneca hapo awali yalifanywa kwa watu wenye umri wa kati ya miaka 18-64 na zaidi ya 65.