Back to top

COPRA, WASAMBAZAJI NGANO WASAINI MAKUBALIANO.

06 August 2024
Share

Mamlaka ya Nafaka na Mazao mchanganyiko (COPRA), Imeingia makubaliano na taasisi zinazohusiana na usambazaji, usindikaji  na uchakataji wa zao la ngano nchini ambayo yatakwenda kuongeza chachu ya uzalishaji wa zao la hilo hapa nchini.


Wamesaini makubaliano  hayo na Mkurungenzi wa Mamlaka hiyo Bi. Irene Mlola katika viwanja wa Nane nane Nzuguni jijini Dodoma, na kushuhudiwa na  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde.

 
Akizungumza katika hafla Hiyo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde Ameipongeza COPRA kwa kusaini makubaliano hayo na kusema hatua hii ni chachu ya wakulima kuchangamkia fursa ya uzalishaji kwa kuwa soko lipo la uhakika.

Kwa upande wake  Mkurugenzi Mkuu wa COPRA Bi. Irene Mlola ametoa rai kwa  wakulima hapa nchini kuzalisha ngano kwa wingi na yenye ubora ili kampuni hizo ziweze kupata ngano ya kutosha  ili kukizi Soko la ushindani.