
Diwani wa Kata ya Nyarukoba wilayani Tarime mkoani Mara, Juma Athuman Matiko Pamoja na Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Marshi ya mjini Musoma, Denis Karume Nyakira wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma kwa tuhuma za ubadhirifu wa shilingi Milioni 80.4 fedha zilizotolewa na Mgodi wa Norh Mara kwa ajili ya ufadhili wa wanafunzi 134.
