Back to top

DKT.MOLLEL: LENGO NI KUFIKIA ZERO MALARIA IFIKAPO 2030

25 April 2024
Share

Kamati za Ulinzi na Usalama nchini, zimetakiwa kuifanya ajenda yakutokomeza Malaria iwe yakudumu kwenye vikao vya maamuzi.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, alipomwakilisha Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kwenye kilele cha Siku ya Malaria Duniani iliyofanyika mkoani Tabora, ambapo ameeleza kuwa nchi imeendelea kupiga hatua katika vita dhidi ya malaria, ikilinganishwa na miaka zaidi ya 20 iliyopita ambapo maambukizi na vifo vilivyotokana na ugonjwa huo vilikuwa kati ya 45% hadi 50%.
.
Dkt.Mollel, amesema lengo la Serikali ni kufikia 3.5% ifikapo 2025 na kuwa na ziro Malaria 2030, huku akisisitiza kuwa kiwango hicho kitafikiwa endapo juhudi za makusudi zitafanywa kwa ushirikiano baina ya Serikali na wadau
.
"Leo tunazungumza asilimia 8.1 kama nchi lakini miaka ya 1998, tulikuwa na kiwango cha juu sana, hivyo ili tuweze kufikia adhma yakumaliza kabisa malaria ifikapo 2030 kila mmoja wetu anawajibu wakufanya" amesema Dkt.Mollel.