Back to top

DONALD TRUMP KUREJESHWA TWITTER

20 November 2022
Share

Mmiliki mpya wa mtandao wa Twitter Elon Musk ametangaza kumrejesha Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump kwenye mtandao huo baada ya kumzuia kutokana na ghasia zilizotokea Januari 06, 2021, ikisema kwamba machapisho yake yalikuwa yakichochea ghasia.
.
Hatua hiyo ya inafuata baada ya Elon Musk kuwataka wafuasi wake kupiga  kura ya maoni akiwauliza kama Trump arudishwe au asirudishwe kwenye mtandao huo, ambapo watu milioni 15 walipiga kura huku 51.8% wakisema arudishwe.
.
Baada ya kura hizo, Musk aliandika "Watu wamezungumza", "Trump atarejeshwa" huku akiongeza usemi wa Kilatini “Vox Populi, Vox Dei,” akimaanisha "sauti ya watu, ni sauti ya Mungu".