Back to top

EWURA KUTATHMINI KUPATA BEI MOJA YA MAFUTA

03 April 2024
Share

Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) inafanya tathmini ya uwezekano wa kupanga bei moja ya bidhaa za petroli nchi mzima.

Naibu Waziri Nishati, Mhe.Judith Kapinga, amebainisha hayo bungeni Jijini Dodoma, katika kipindi cha maswali na majibu, akijibu swali la Mbunge wa Arusha Mjini Mhe.Mrisho Gambo, kuhusu mkakati wa serikali kutafutia ufumbuzi suala hilo.

Utaratibu huo ambao ulikuwa ukitumika miaka ya nyuma, ulikwama kutokana na uwepo wa changamoto za kisera na za kiusimamizi, hatua ambayo iliruhusu wafanyabiashara wa mafuta kupanga bei za bidhaa za mafuta kuendana na ushindani wa soko.

Tathmini hiyo itakapokamilika, serikali itajiridhisha iwapo utaratibu huu una tija ,ikiwa ni pamoja na kujua namna bora ya kuhusimamia, ili kuhakikisha changamoto zilizojitokeza nyuma hazijirudii.